ERIKA KIRK AISHANGAZA DUNIA KWA UJUMBE WA MSAMAHA
Na Dotto Kwilasa
Katika mazishi ya mumewe Charlie Kirk yaliyohudhuriwa na zaidi ya watu 90,000 kwenye State Farm Stadium, Arizona, Erika Kirk aliibua hisia nzito baada ya kutangaza hadharani kumsamehe kijana anayetuhumiwa kumuua.
Erika alisema anachagua upendo na msamaha badala ya chuki, akisisitiza kuwa huo ndio urithi aliouacha mumewe.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi wakuu akiwemo Rais wa zamani Donald Trump na Makamu wa Rais JD Vance, ambao walimtaja Charlie kama shujaa wa imani na sauti ya vijana Marekani.
Charlie Kirk, mwanzilishi wa Turning Point USA, aliuawa Septemba 10 akiwa na umri wa miaka 31, na baada ya kifo chake mkewe Erika aliteuliwa kuwa CEO wa shirika hilo.
Hotuba ya msamaha wa Erika imegeuka gumzo duniani, ikielezwa na wataalamu kama mfano wa imani na uthabiti wa kimaadili.


No comments