Header Ads

DOTK-BAR

Kyara wa SAU Aahidi Ajira Milioni 10 kwa Vijana



Na Hamis Daud,Dodoma


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara, amechukua rasmi fomu ya kugombea, akiwa na makamo wake wa Rais, Satia Mussa Bebwa ambapo amesisitiza kuwa kipaumbele chake kikuu ni kuunda ajira milioni 10 kwa vijana ndani ya miaka mitano, hatua inayolenga kumkomboa Mtanzania na kuhakikisha fursa za ajira zinagusa kila kaya.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kyara amesema: “Ajira ni msingi wa maendeleo,tunataka kila kijana awe na nafasi ya kufanya kazi, kujitegemea na kuchangia uchumi wa taifa hiki ndiyo kipaumbele chetu, "amesena

Mgombea huyo aliweka wazi kuwa sera yake ya ajira itaangazia pia kupunguza ajira zisizofaa kwa watoto wa kiume na kuhakikisha vijana wanapata mafunzo na ujuzi unaohitajika sokoni.

Mbali na ajira, Kyara ametaja kipaumbele chake cha pili kuwa ni nishati safi, ambapo serikali yake itashirikiana na kampuni za kutengeneza majiko ya kisasa yanayotumia nishati rafiki kwa mazingira.

Lengo ni kupunguza gharama za umeme, kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa wananchi wa pembezoni, na kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi za kupikia.

Aidha, Kyara amesisitiza sera za kuhakikisha bei za mafuta kwa wananchi wa pembezoni ziwe nafuu na kurekebisha maslahi ya walimu, ikiwa ni pamoja na mishahara ya wakati na mazingira bora ya kufundishia.

“Tunahitaji walimu wenye motisha, shule zenye miundombinu bora na vitabu vya kufundishia vya kisasa,” ameongeza.

Mgombea huyo amesisitiza pia kurejesha mchakato wa katiba mpya, akisema: “Tunakwendza kuzindua katiba mpya ndani ya siku 40, kuunda serikali yenye uwazi, haki na maendeleo endelevu.”

Hatua hii inahusiana na azma yake ya kujenga serikali ya watu wenye hofu ya Mungu, yenye uadilifu unaotakiwa na wananchi. 

Amesema baada ya kuchukua fomu, yeye na timu yake wanakusanya wadhamini ili kuanza rasmi kampeni, huku wakisisitiza kuwa serikali yao italeta mapinduzi ya kiuchumi, ajira kwa vijana, na matumizi ya nishati safi kwa manufaa ya wananchi wote.






No comments

Powered by Blogger.